Ibada ya Dua’u al-Nudba inabeba nafasi maalum katika maisha ya Waislamu, hususan wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s), kwani ni dua inayokumbusha mapenzi, hamu na matarajio ya muumini kwa kuonekana kwa Imam wa Zama (a.t.f.s) na kushamiri kwa haki duniani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Leo tarehe: Ijumaa, 11 Rabiul Thani 1447 H / 3 Oktoba 2025 Ijumaa alfajiri imefanyika ibada tukufu ya Dua’u al-Nudba katika Madrasa ya Mabinti wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (a.s) iliyopo Kigamboni, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ibada hiyo ilianza mara baada ya Swala ya Alfajiri na ilidumu kwa takribani dakika 40, huku wanafunzi wote wa madrasa wakishiriki kwa unyenyekevu pamoja na walimu wao. Shughuli hii ya kiroho ilihusisha kusomwa kwa maneno matukufu ya Dua’u al-Nudba, ambamo waumini hujielekeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu (SWT) na kumuomba kupitia maneno yaliyojaa hekima na mapenzi ya Ahlul-Bayt (a.s).
Kwa utaratibu wa kila Ijumaa, wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Kidini kilichopo chini ya madrasa hii hufanya ibada hii, ambayo inalenga:
1_ Kuimarisha hali ya kiroho na maadili ya kidini kwa wanafunzi.
2_Kukuza mapenzi na mawadda kwa Ahlul-Bayt (a.s) kupitia dua na mafundisho yao.
3_Kuendeleza ukuzaji wa elimu ya kiroho na kujikurubisha zaidi kwa Allah (SWT).
4_Kuimarisha uhusiano wa kiimani na Imam wa Zama, Imam Mahdi (a.t.f.s).

Your Comment